Aliyekuwa Katibu Mkuu (OMKR)
Khadija Kamis Rajab (kushoto) akimkabidhi nyaraka na vitabu mbalimbali Katibu
Mkuu (OMKR) Omar Dadi Shajak (kulia) ikiwa na maana ya kumkabidhi Ofisi hiyo
rasmi, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamo wa
Kwanza wa Rais Kilimani Mjini Unguja. Katikati ni Waziri wa Nchi (OMKR) Saada
Mkuya Salum.Ameyasema hayo huko
katika ukumbi wa Ofisi hiyo iliyoko Migombani wakati wa makabidhiano ya Ofisi
kwa Makatibu wakuu na kuwataka kushirikiana katika utendaji wa kazi na
kuwakaribisha na kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Amesema muelekeo wa
kazi katika wizara hiyo unakwenda vizuri hivyo amewasisitiza kuwa nae karibu
katibu mpya katika kutekeleza majukumu ya Serikali ambapo inahimiza kila
mfanyakazi kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Aidha amemshukuru
katibu anaeondoka kwa alivyofanya kazi zake kwa na kumuomba anakokwenda
akayatimize wajibu na uimara wake kama alivyoyafanya hapo.
Nae Katibu Mkuu Kazi
na Uwezeshaji Khadija Khamis Rajab amesema kwa muda aliofanya kazi ameweza
kupata mafanikio ikiwemo kupata ofisi ambapo hapo mwanzo kulikuwa kuna ufinyu
na kuweza kupunguza baadhi ya madeni ya wafanyakazi yakiwemo wanayodai Pesa
za likizo na mambo mengineo.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais Omar Dadi Shajack ameahidi kufanya
kazi kwa mashirikiano ili majukumu ya kazi yaweze kuendelea ikiwemo uwajibikaji
kwa kila mmoja.




0 Maoni