Na mwandishi wetu
Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika kujipatia kipato cha halali kwa lengo la kupunguza changamoto ya upatikanaji wa ajira inayozikumba nchini nyingi arani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Khamis Hamza Chilo ametoa wito huo wakati akifungua kongamano maalum la kutimia miaka mitano tokea kuasisiwa kwa Wazalendo Company Limited lililofanyika katika viwanja vya Mau Zi-tong jijini Zanzibar.
Amesema Serikali zote mbili ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweza kuinua hadhi ya vijana kwa kutoa kipaumbele maalum katika maeneo mbali mbali ikiwemo nafasi za uongozi.
Amesema katika kulitekeleza kwa vitendo serikali zote mbili kwa asilimia kubwa imeteuwa viongozi vijana kutokana na kuunga mkono na kuthamini jitihada za vijana katika kuchangia maendeleo ya Tifa.
Aidh Mhe. Chilo amewashauri vijana hao kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini ili kujenga mustkbali mzuri wa serikali kuwafikishia maenedeleo wananchi wake.
yapo mataifa kadhaa duniani yamekosa Amani na kusababisha wananchi wake kuwa wahanga na kukosa kutekeleza mahitaji yao ya msingi huku akionya kuwa Serikali haitomvumilia mtu yoyote yule atakaejaribu kuvunja amani iliyopo.
Akigusia suala la mikopo ya elimu ya juu Mhe. Chilo amesema Serikali imeongeza bajeti kwa Wizara ya Elimu ili kjutoa fursa kwa vijana kusoma bila ya kikwazo chochote, na kuwataka kuwa wepesi kurejesha mikopo mara wanapomaliza masomo yao ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wengine kukopeshwa.
Akigusia kuhusu uzalendo Mhe Chilo amewataka vijana hao kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali, ikiwemo kulitumia Baraza la Vijana Zanzibar ili kuweza kufikisha changamoto na mawaoz yao katika kuijenga Zanzibar Mpya.
Nae Mkurugenzi wa Wazalendo Company Limited Ndugu Masoud Ali Juma amesema lengo la kuandaa kongamano ni kuweza kutoa fursa kwa vijana kujadili kwa pamoja namna bora ya kuweza kujikwamua kimaisha na kuweza kujiajiri pindi wanapomaliza masomo yao.
Akiwasilisha mada katika Kongamano hilo Dk. Suleiman Haji amewashairi vijana waliopo vyuoni kuweka malengo ya kujiendeleza zaidi baada ya kumaliza masomo yao katika ngazi walizokuwepo sasa.
Nae Katibu Mtendjai wa Baraza la Vijana Taifa Ndugu Salum Issa Ameir amewataka vijana hao kutumia elimu na ujuzi waliokuwa nao ili kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kuyatumia mafunzo vizuri walioyapata Vyuoni.
ANGALIA VIDEO YA TUKIO ZIMA ZILIVYOKUA KATIKA KONGAMANO LA FUSRA LILILOANDALIWA NA WAZALENDO C LTD





0 Maoni