Mbunge wa Jimbo la Uzini ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamis Chilo amesema uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji unasababisha baadhi ya kesi za udhalilishaji kuchukua muda kukamilika ushahidi wake jambo ambalo linawaumiza wananchi

Mhe Chilo ameyasema hayo jana(Augost 10) wakati akijibu malalamiko ya wananchi katika Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Adid na kushirikisha wananchi kutoka Shehia zote Nne za Jimbo la Uzini kwaajili ya kuskiliza kero za wananchi na kuzipatia Ufumbuzi

Amesema  hakuna sababu katika Kesi ya Mtoto aliekutwa  amedhalilishwa na  upelelezi wake ukafika miezi sita au saba wakati ushahidi uanonyesha wazi kuwa mtoto ameharibiwa.

 ‘‘unajua kuna mambo mengine kama kuna baadhi ya watu wanazembea zembea, hakuna sababu  kesi ya mtoto aliezalilishwa kesi ikafika miezi saba au nane, wakati ushahidi upo maana umemkuta hasa mtoto ameharibiwa ushahidi wote upo alafu unaendelea kupeleleza, kupeleleza et ushahidi haujakamilika ,ushuhudie nini’’amesema Mhe Chilo.

Katika mkutano huo Mhe Chilo amemuahidi Mkuu wa Mkoa kukaa na watendaji wa Jeshi la Polisi kwaajili ya kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto hizo.