Naibu Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akikagua sifa
(specifications) na ubora wa moja ya kompyuta 19 zilizonunuliwa katika
Telesenta ya Sengerema kwa ufadhili wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Richard
Na mwandishi wetu
Watumishi watatu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wanaosimamia Redio Sengerema 98.8 FM
wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa ubadhirifu wa shilingi Milioni Ishirini na
Saba laki Saba na Elfu Ishirini (27,720,000).
Fedha hizo zilizopotea ni
bakaa ya shilingi Milioni 103 zilizotolewa na taasisi ya mawasiliano ya Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajili ya kuboresha Telesenta ya Sengerema
Maamuzi hayo yametolewa
na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew
baada ya kufika katika Telesenta hiyo na kusomewa taarifa ya matumizi ya fedha
hizo iliyoonesha kuna bakaa ya shilingi Milioni 27,720,000 huku taarifa ya
kibenki ya akaunti ya kituo hicho ikionesha fedha zote zimetumika na hakuna
bakaa yeyote
Aidha, baada ya
Mhandisi Kundo kuhoji kwanini taarifa ya kibenki inakinzana na taarifa
waliyomsomea ndipo Meneja wa Kituo hicho Sostenes Tangalo kukiri kuwa wakati
kituo kinapatiwa fedha na UCSAF suala la kurekebisha studio ya redio halikuwepo
lakini katika manunuzi hayo ambayo yalifanyika kwa malipo ya fedha taslimu
yaani cash wao wakaona wanunue na vifaa vya kurekebisha studio hiyo
pamoja na samani
Baada ya maelezo hayo kuonesha kuna harufu ya ubadhirifu wa fedha za Serikali zilizotolewa na taasisi ya UCSAF ambayo ipo chini ya Wizara hiyo Mhandisi Kundo ameagiza Meneja wa Kituo hicho Sostenes Tangalo, mwanasheria Ilambona Mahuba na Afisa Habari kuwekwa ndani na taratibu za kisheria zifuatwe.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akipitia taarifa ya manunuzi ya vifaa vya kituo Telesenta ya Sengerema. Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Albert Richard






0 Maoni