Wafanyabiashara soko wa soko la muda la Kibanda Maiti wameziomba mamlaka zinazohusika kulifanya soko hilo kuwa la kudumu hatua itakayowapa uhakika wa kuwekeza mitaji mikubwa zaidi sokoni hapo.

Baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapo wameieleza sknews kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uhaba wa wateja na mnada sokoni hapo kuwa ndogo ambapo wameomba kuwekewa soko la kudumu ambalo litaingiza magari ya abiria ambayo yataleta unafuu upande wao.

Akizungumzia ombi hilo, Mkuu wa soko la muda la Kibandamaiti, Juma Ammbar Abeid amesema wanalifanyia Kazi swala hilo na kuwataka wafanya biashara hao kuwa na subra.