Vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto vimeelezwa kuongezeka kisiwani Zanzibar kwa Mwezi Julai hali inayotishia ustawi wa watoto.

Mtakwimu Ramla Hassan Pandu kutoka afisi ya mtakwimu mkuu wa Serikali kitengo cha makosa yajinai, madai na jinsia amesema jumla ya matukio 108 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa ndani ya mwezi wa Julai 2021 idadi ambayo imeongezeka ikilinganishwa na mwezi wa Mei 2021 makosa 97.

Amefahamisha kuwa, Wilaya ya Magharibi A imeripoti makosa 29 ambayo ni mengi zaidi kwa mwezi Julai ikilinganishwa na Wilaya nyengine ikifuatiwa na Magharibi B (23).

Nae Mkurugenzi Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nasima Chum amesema kumezuka wimbi la utoroshaji wa watoto wa kike kuanzia miaka 14 na 17 hivyo ni vyema wazazi kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo kwa kutambua nyendo zao kwa kuanza kuzuia na sio kuondosha.

Nae wakili wa Serikali,  Khamis Othman kutoka afis ya Mkurugenzi wa mashtaka amesema vitendo vingi vya udhalilishaji vinachochewa  na utumiji wa madawa ya kulevya kwa vijana  hivyo huchangia kufanya vitendo vya udhalilihsaji