Mjumbe wa Kamati ya halimashauri kuu ya CCM taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitoa hotuba yake wakati akiyafungua mafunzo elekezi kwa viongozi wa Jumuiya ya wazazi wilaya Mjini yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa SUZA Kampasi ya Maruhubi.
 
Viongozi na Wanachama wa Jumuiya ya wazazi ya Mjini wakifuatilia hotuba ya mjumbe wa Kamati Kuu Mhe. Hemed wakati akiyafungua mafunzo elekezi kwa viongozi  yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa  SUZA Kampasi ya Maruhubi.

 Na mwandishi wetu

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Kichama Visiwani Zanzibar, wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, miiko pamoja na misingi ya chama hicho sambamba na kufanya kazi kwa mashirikiano ili kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halimashauri kuu ya CCM taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameeleza hayo katika Mkutano maalum uliwashirikisha wajumbe wa halimashauri ya Mkoa, wilaya, mabaraza ya Jumuiya za chama cha Mapinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Dimani uliopo Kiembesamaki.

Ameeleza  Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wana jukumu la kuisimamia Serikali katika kuhakikisha ilani ya CCM 2020/2025 inatekelezwa vyema na viongozi wanatekeleza miradi mbali mbali iliopo Serikalini.

Aliewaleza viongozi hao wa chama kwamba, wasisite kuitembelea na kuikaguwa miradi inayotekelezwa na serikali katika ngazi za wilaya na Mkoa pamoja na kutoa maelekezo pale inapohitajika lengo likiwa ni kuhakikisha ahadi zilizotolewa na viongozi wakadi wakiinadi ilani hiyo zinatakelezwa kwa vitendo.

Mjumbe huyo wa Kamati kuu alisema bajeti ya serikali iliopitishwa karibuni na wajumbe wa baraza la wawakilisha inalenga kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili wananchi wake pamoja na kuwaletea maendeleo.

Mapema, Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halimashauri kuu ya CCM taifa alifungua mafunzo elekezi ya vionjgozi wa Ngazi ya matawi, wilaya kwa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Mjini yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha SUZA kamapasi ya Maruhubi.

Akiyafungua mafunzo hayo, Mhe. Hemed alitoa wito kwa Jumuiya za Chama kubuni miradi itakayosaidia Jumuiya hizo kujijenga Kiuchumi ili ziweze kujitegemea kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama cha Mapinduzi.