Balozi Irene Kasyanju (kulia) akiangalia namna uyoga
unavyofungashwa kwenye makasha (packaging) tayari kwa kupelekwa sokoni huku
akipatiwa maelezo ya mchakato mzima wa ufungaji kutoka kwa Mkurugenzi
Mwendeshaji wa LIMAX Group Bw. Rob Menheere (kushoto). Katikati ni Bw. Petro
Mahuwi “intern” Mtanzania aliyeongozana na Balozi Kasyanju kwenye ziara hiyo.Kampuni maarufu ya Uholanzi, LIMAX B.V.
(LimaxGroup) imedhamiria kuwekeza kwenye Sekta ya Uyoga nchini Tanzania kwa
kujenga kiwanda cha kusindika na kukausha uyoga Mkoani Iringa kwa thamani ya
Euro milioni 2.1 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 5.5 za Tanzania.
Hayo
yameelezwa kufuatia Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju
kutembelea kampuni hiyo tarehe 26 Agosti 2021 na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi na Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Tom VanWalsem.
Balozi Kasyanju ameeleza kuwa uwekezaji huo
utakapokamilika, Tanzania itafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na mtiririko wa
biashara ya uyoga kukua kwa kasi duniani ambapo kwa mujibu wa Shirika la
Chakula na Kilimo (FAO), biashara hiyo inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia Dola
za Marekani bilioni 62.2 ifikapo mwaka 2023 kutoka Dola za Marekani bilioni
42.4 mwaka 2018.
Balozi Kasyanju akiwa katika kampuni hiyo alipata
fursa ya kujionea mashamba ya kisasa ya uyoga unaozalishwa (sio wa asili) na namna
zao hilo lenye faida kubwa kwa binadamu linavyosindikwa na kufungashwa
(processed and packed) na kuelezea matumaini yake kuwa Tanzania itafaidika na
uwezo, uzoefu na utaalam mkubwa wa biashara wa Kampuni hiyo.
Namna kitalu kimoja
wapo cha uyoga uliopandwa na ambao unakaribia kuvunwa kinavyoonekana katika
moja ya mashamba makubwa 4 ya LIMAX Group iliyoko Horst, Uholanzi.



0 Maoni