Na mwandishi wetu
Makatibu Wakuu wa Wizara za Afya pamoja na Wataalam
wa Wizara hizo kutoka Tanzania na Kenya wamekutana jana jijini Nairobi kujadili
changamoto za masuala ya Corona kwa upande wa kibiashara upande wa mipakani mwa
nchi hizo.
Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha awali cha
wataalum wa sekta hiyo na baadae kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu hao
ambao wamejadiliana masuala ya upimaji wa Corona baina ya nchi hizo mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Tanzania, Prof. Abel
Makubi amesema mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Marais wa
nchi hizo mbili walipokutana mwaka huu jijini humo.
Ametaja baadhi ya mambo waliyoyajadili ni pamoja na
kuhakikisha kunakuwa na mifumo inayoweza kuwasiliana katika upimaji kwa kuweza
kuonekana kwa upande wa Tanzania na wakati huo huo kwa upande wa Kenya.
Kwa upande wa gharama za upimaji hususan kwa
madereva wa magari makubwa, amesema wamejadili na kutoa mapendekezo
yatakayopekekwa kwenye kikao cha Mawaziri wa nchi hizo mbili siku ya Alhamisi
kupata maamuzi ya mwisho.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Kenya. Susan
Mochache amesema wamejadili kurahisisha biashara kati ya nchi hizo mbili
ikiwemo kupitisha mizigo tofauti ikiwemo chakula.





0 Maoni