Waziri wa Maji na Nishati Zanzibar Mhe Sleman Masood (wa kati) akiwa katika ufunguzi wa Kikundi cha Baba na Mama lishe Kiwengwa ,Mh Asha Abdallah Musa  (wa kwanza kushoto) Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda  Mstahiki Meya Magharib B (wa kwanza kulia)
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Asha abdallah Musa

Na Suleiman Mohamed

Waziri wa Maji na Nishati Zanzibar Mh Slemani Masood Makame amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga kuondosha Changamoto ya upatikanaji wa Maji safi na salama  kwa wananchi wa maeneo yote hasa katika maeneo ya Makazi na uwekezaji.

Mhe Sleman ameyasema hayo kiwekwanga Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wa Uzinduzi wa Kikundi cha Baba lishe na Mama lishe wa Kijiji cha Kiwengwa mafarasi ambapo wanakikundi hao walilalamikia changamoto ya upatikanaji wa maji .

Amesema Serikali itapita katika maeneo yote yenye changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama na kubaini kasoro zilizopo ili waweze kuzifanyia kazi kwaajili ya kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana katika maeneo yote ya Zanzibar ikiwemo Kiwengwa.

Kuhusiana na kikundi hicho Mhe  Sleman amesema yuko tayari kushirikiana na mwakilishi wa Jimbo hilo kuhakikisha wanatoa msaada wa kukiweshesha kikundi hicho kisajiliwe ili waweze kunufaika na fursa mbali mbali Serikalini ikiwemo mikopo kwaajili ya kuendeleza kikundi.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda  Asha Abdallah Mussa amesema atahakikisha anaishauri Serikali ili mfuko wa uwezeshaji Kiuchumi kutoka Wizara husika unasimamiwa ipasavyo ili uweze kuwanufaisha wananchi kama lengo lilivyokusudiwa.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wanakikundi cha Baba lishe na Mama lishe Mariamu Juma (kitam) amesema changamoto inayowakabili kikundi hicho ni Upatikanaji wa Maji safi na Salama kwaajili ya kuendeleza biashara zao hali inayopelekea kununua Dumu moja la Maji kwa shilingi elfu moja (1000) jambo walilolieleza linarudisha nyuma juhudi zao.

Katika hafla hiyo Mwakilishi wa Jimbo hilo Asha Abdallah Mussa ametoa kiasi cha shilingi laki Tano taslim (500,000) kwaajili ya kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya hamsini tokea kuanzisha kwakwe mwezi june 2021.

picha ya Pamoja Mhe waziri,Mwakilishi,Meya na wanakikindi wa baba lishe na mama lishe Kiwengwa Mafarasi
                  madensa kutoka kikundi cha Wanyambi Mahonda walionesha burudani
Mwakilishi jimbo la mahonda akimweleza jambo Mgeni Rasmi Mh Sleman Masood

Wanakikundi cha Baba Lishe na Mama lishe Kiwengwa wakifuatilia shuhuli ya ufgunguzi wa kikundi chao