Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba Leo August 31,2021 ametia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021 na kupunguza viwango vya tozo za miamala kwa 30% huu ukiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia ambaye alielekeza tozo zipitiwe upya baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu tozo hizo.
Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa Tangazo la Serikali kesho September 01,2021 ambapo Serikali imesema inaamini uamuzi huo utatoa nafuu kwa Wananchi na kuiwezesha Serikali kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyokusudiwa wakati tozo hizo ziliporidhiwa na kupitishwa na Bunge la Bajeti la Mwaka 2021/2022.






0 Maoni