Mhe. Hemed akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Mjini (Hawapo Pichani) katika Mkutano Mkuu maalum uliofanyika katika Ukumbi wa Amani CCM Mkoa ambapo amewahakikishia wanachama hao kuwa serikali itaendelea kudhibiti mfummko wa Bidhaa Nchini

Na mwandishi wetu 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeitaka Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar,  kuweka bei elekezi katika baadhi ya bidhaa muhimu ili kuepusha kuwaumiza wananchi hasa wa hali za chini.

Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar  Hemed Suleiman Abdulla wakati akitolea ufafanuzi malalamiko ya baadhi ya viongozi wa chama hicho walio kuwa wakiiomba Serikali kuangalia upya suala la upandaji wa bei kwa baadhi ya bidhaa muhimu ikiwemo mchele,unga na mafuta katika kikao Cha Viongozi na Wanachama wa CCM Mkoa Mjini kilichofanyika katika ofisi za CCM Amani Agosti 8-2021

Mhe Hemed amesema Serikali haitomvumilia mfanyabishara yoyote atakaekwenda kinyume na bei elekezi zinazotolewa na Serikali na atakaebainika kutenda kosa hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katika hatua nyengine Mhe Hemed amewaomba viongozi hao wa CCM kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa katika mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya ili kujenga Taifa lenye Afya bora na kupata viongozi bora  wa baadae.

Amesema Serikali itachukua hatua kali ikiwemo kufanya marekebisho ya baadhi ya Sheria kwa lengo la kuwadhibiti wale wote wanaojihusisha na vitendo haramu vya kuharibu jamii ya wazanzibar.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Talib Ali alimueleza Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM Taifa kuwa katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa mara ya kwanza Mkoa huo kuchukua ushindi wa majimbo yote kwa nafasi zilizogombewa.


Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa Mjini wakifuatilia hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu Mhe. Hemed alioitoa katika Ukumbi wa Amani CCM Mkoa.
Mjumbe wa Kamati Kuu Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini wa Mjini wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa CCM Amani Mkoa kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa Chama wa Mkoa huo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kuimarisha Chama.