Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili Sylevester Nyegu na Daniel Mbura.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira
Amworo amesema baada ya kusikiliza ushahidi wote na upande wa mashtaka.
Mahakama imebaini washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.
Hakimu Amworo amewaambia washtakiwa hao kwamba
wanaruhusiwa kujitetea Mahakamani hapo kwa njia ya kiapo au bila kiapo.
Aidha Mahakama imewataka washtakiwa kutaja idadi ya
mashahidi na vielelezo watakavyokuwa navyo na kwamba utetezi wao utaanza
kusikilizwa hapo kesho Agosti 13.
Sabaya na wenzake wawili wanashtakiwa kwa makosa
matatu ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha. Kesi hiyo inayowakabili
ilifunguliwa Mahakamani hapo Julai 16 na kuanza kusikilizwa Julai 19 mwaka huu.





0 Maoni