Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti leo
(04.08.2021) amewaongoza wananchi wa Mkoa huo kupata chanjo ya kinga dhidi ya
Ugonjwa wa Virusi vya Corona ambapo amesema kuwa chanjo hiyo ni Salama na
inalenga kuwasaidia watu kuwa na kinga imara .
Amesema Wananchi wa Mkoa wa Rukwa ni vema wakajitokeza kupata chanjo jiyo dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona ambapo Serikali Mkoa wa Rukwa imeanza kutoa chanjo kwa wananchi wenye uhitaji wa Chanjo hiyo kwa hiyari.
Mkiritiki amewaeleza wakazi wa Sumbawanga waliokusanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imethibitisha pasipo shaka kuwa chanjo hii ya UVIKO 19 ni salama na kuwataka wengi wajitokeze kupata chanjo hiyo.
"Rais Samia amesema chanjo hii ni bure na ya hiari kwa mwananchi yeyote mwenye kuhitajinili kujikinga na ugonjwa wa Corona. Mimi leo nitakuwa wa kwanza kuchanja hapa hapa " alisema Mkirikiti
Akizungumza kuhusu chanjo hiyo Mganga Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu alisema lengo la serikali kutoa dozi hizo za chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona utasaidia kuongeza kinga ya mwili ya mwanadamu .
Aliongeza kusema lengo jingine ni kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa pia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona.
"
Tumepokea dozi za chanjo Elfu Ishirini ambazo tayari zimefikishwa kwenye vituo
11 vilivyoanishwa kutoa chanjo, wananchi naomba tujitokeze kupata chanjo"
alisema Dkt. Kasululu
baadhi ya Wanachi waliojitokeza kupata Chanjo ya Uvico 19 Katika Hospitali ya Mkoa Sumbawanga







0 Maoni