Mkuu wa Mkoa Kusini
Unguja Rashid akizungumza na wananchi wa Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini UngujaNa mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa Kusini
Unguja Rashid Hadid amesema Serikali ya Mkoa imedhamiria kushuhulikia
kikamilifu changamoto zinazokabili Mkoa huo ikiwemo uuzaji na utumiaji wa
madawa ya kulevya, wizi wa mazao na suala ya udhalilishaji
Mhe Hadid ametoa
kauli hiyo jana (August 10) katika Shehia kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
alipokutana na wakaazi wa Shehia Nne za Jimbo la Uzini kwa ajili ya kusikiliza
kero zinazowakabili katika vijiji vyao ambapo amesema hadi sasa tayari ameshapata
orodha ya majina ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya na amedhamiria
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusishwa katika ripoti yake.
Katika hatua nyengine Mh Hadid Amesem Serikali
haitasita kuendelea kuyafanyia uchunguzi majina ya watu wa
jimbo la uzini ambao wanajihusisha na vitendo
vya udhalilishaji na wizi wa mazao.
Amesema Jambo la
udhalilishaji ni baya hivyo ni vema wananchi wakashilikiana na Viongozi wa
Serikali ikiwemo Masheha katika kujenga nidhamu na Maadili mema katika Jamii
Kwaupende wao
Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo hilo amemweleza mkuu wa mkua juu ya kufahamu changamoto zinazokabili Jimbo hilo na
kuahidi kushirikiana na wananchi katika kupata ufumbuzi wa changamoto hizo
Katika kushuhulikia
changamoto hizo kwa Vitendo Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja ametoa wito wa kuundwa
kwa Kamati za Ulinzi shirikishi katika shehia ili kushirikiana kwa pamoja
kuondoa changamoto zinazokabili Jimbo hilo.




0 Maoni