Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 16 Agosti, 2021 anatarajia kuondoka Jijini Dodoma kuelekea nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC utakaofanyika kuanzia tarehe 17 – 18 Agosti, 2021.

Katika Mkutano huo wa 41 pamoja na mambo mengine, Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, watathibitisha nchi ya Malawi kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja (Agosti 2021 – Agosti 2022).

Matangazo ya kuwasili Mhe. Rais Samia nchini Malawi na Mkutano huo yatatangazwa moja kwa moja (Mbashara), kupitia Youtube Channel ya Ikulu Mawasiliano na Runinga mbalimbali nchini.