Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya
kuratibu Mpango wa kuitangaza Tanzania kimataifa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi, amesema Mhe. Rais Samia
atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya utalii,
uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo
nchini.
Mhe. Rais Samia na wageni hao wa Royal Tour wameanza zoezi hilo la
kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji tarehe 28 Agosti,
2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar.





0 Maoni