Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa
na marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha katika
Serikali ya Awamu ya Tatu, Marehemu Basil Mramba kilichotokea
tarehe 17 Agosti, 2021 katika Hospitali ya Regency Jijini Dar es
Salaam.
Mhe. Rais Samia amesema katika kipindi cha uhai wake Marehemu
Basil Mramba alitoa mchango mkubwa kwa taifa na atakumbukwa
kwa yale yote mazuri aliyoyafanya katika utumishi wake .
“Nimesikitishwa sana na kifo cha Marehemu Mramba, nawaombea
wafiwa wote wawe na moyo wa subira, uvumulivu na ustahimilivu
katika kipindi hiki cha majonzi cha kumpoteza mpendwa wao”
amesema Mhe. Rais Samia.
Mhe. Rais Samia pia amemuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe
roho ya Marehemu mahali pema Peponi, Amina.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe




0 Maoni