Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:-
1. Amemteua Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU)
amememteua Prof. Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Prof. Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (upande wa Mifugo)
Prof. Ole Gabriel
anachukua nafasi ya Bw. Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu. Prof. Ole Gabriel ataapishwa tarehe 21
Agosti, 2021, saa 03:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam pamoja na Mabalozi
Wateule watatu (03) kama ifuatavyo:-
1.
Balozi Mteule Lt. Jen. Yakub Hassan
Mohamed kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki.
2.
Balozi Mteule Mahmoud Thabit Kombo kuwa
Balozi wa Tanzania nchini Italia.
3. Balozi Mteule Elsie Sia Kanza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.





0 Maoni