Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan leo tarehe 03 Agosti, 2021 amehitimisha Ziara yake ya siku mbili
nchini Rwanda kwa kutembelea viwanda vitatu na kujionea shughuli mbalimbali za
uzalishaji zinazofanywa na viwanda hivyo.
Katika kiwanda cha kwanza cha Inyange
kinachotengeneza vinywaji, Mhe. Rais Samia akiwa na mwenyeji wake Rais wa Rwanda
Mhe. Paul Kagame wamejionea shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwa
ni pamoja na maji ya kunywa, maziwa na juisi.
Aidha, Mhe. Rais Samia pia ametembelea kiwanda cha
kutengeneza simu za mkononi cha Mara Phone na kujionea hatua mbalimbali za
utengenezaji wa simu kuanzia hatua ya awali hadi kukamilika kwake.
Pia Mhe. Rais Samia ametembelea kiwanda cha
uunganishaji magari cha Volkswagen
kilichopo nchini humo na kujionea hatua mbalimbali za kuunganisha magari hayo
ambayo huuzwa nchini humo.
Mhe. Rais Samia amewaagiza Waziri wa Viwanda na
Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe
kukutana na wamiliki wa viwanda hivyo ili kutumia fursa zilizopo katika viwanda
hivyo ikiwa ni pamoja na kuwauzia malighafi zinazopatikana nchini Tanzania.
Mhe. Rais Samia ameagana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul
Kagame katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali na kurejea Jijini Dar es
Salaam baada ya kumaliza Ziara Rasmi ya siku mbili nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja
na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakiangalia baadhi ya Bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa katika kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini
Kigali wakati walipotembelea kiwanda hicho leo tarehe 03 Agosti,2021Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na
mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakitembelea katika kiwanda cha
Inyange Plant Entrance mjini Kigali kinachozalisha Juisi, Maziwa na Maji ya
kunywa leo tarehe 03 Agosti,2021.
0 Maoni