Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 06 Agosti, 2021 amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-
1.
Amemteua Bw.
Athumani Seleman Mbuttuka kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (Internal Auditor General).
Bw. Mbuttuka anachukua nafasi ya Balozi Mohamed Mtonga ambaye amestaafu
na Balozi wa Tanzania nchini Qatar. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mbuttuka alikuwa
Msajili wa Hazina (Treasury Registrar).
2. Amemteua Bw. Leonard John Mkude kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali (Accountant General). Bw. Mkude anachukua
nafasi ya Bw. Francis M. Mwakapalila ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya
uteuzi, Bw. Mkude alikuwa Meneja Bajeti, Benki Kuu ya Tanzania.
3. Amemteua Bw. Mgonya A. Benedict kuwa Msajili wa Hazina.
Bw. Benedict anachukua nafasi ya Bw. Athumani Mbuttuka ambaye ameteuliwa
kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Benedict
alikuwa Meneja wa Masuala ya Fedha na Madeni, Benki Kuu ya Tanzania.
4. Amemteua Bw. Frank Mugeta Nyabundege kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (Tanzania
Agriculture Development Bank). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Nyabundege alikuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Lake Oil Tanzania
Limited.
5. Amemteua Bw. Casmir Kyuki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya
Uwekezaji ya UTT – AMIS. Bw. Kyuki ni Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria
Tanzania.
Teuzi hizi zimeanza tarehe 05 Agosti, 2021.





0 Maoni