Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameivunja bodi ya Kampuni ya uvuvi Zanzibar
ZAFICO kuanzia leo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Katibu wa Baraza la
Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mussa Haji Ali amesema Rais Dkt.
Mwinyi ameivunja bodi hiyo iliyoanza majukumu yake Juni 9/ 2021.
ZAFICO ni kampuni ya uvuvi Zanzibar iliyo chini ya
Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ilianzishwa na kuanza kazi Mwezi Oktoba
2017.




0 Maoni