Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja imeeleza kukabiliwa
na ongezeko la wagonjwa wa Covid 19 Hospitalini hapo hali inayosababisha uwepo
wa changamoto ya uhitaji mitungi ya gesi
ya Oksjeni zaidi kutokana na ongezeko la
Wagonjwa hao wa Covid 19.
Akizungumza na sknews kwa njia ya simu Msemaji wa
Hospitali ya Mnazi mmoja Hassan Makame amesema Jumla ya Mitungi Mia Nne (400)
inahitajika ili kukabiliana na mahitaji wa wagonjwa waliopo hivi sasa.
Amesema mitungi ya Oksijeni kwa sasa imekua ikiwalazimu
kuagiza kutoka Dar es salaam kutokana na
hospitali hiyo mtambo wake wa kuzalisha mitungi hiyo kutokidhi kwakua uzalishaji
wake ni mitungi 30 kwa siku idadi ambayo ni ndogo ukilingalisha na mahitaji ya
Wagonjwa.
" kwa sasa mitungi tulionayo haizidi mia mbili
na kidogo na sisi hapa tunatumia mitungi mia kwa siku, tunahitaji walau kama
hatuna mingi tupate mitungi walau mia nne''
Hassan Makame amesema licha ya Mtambo wa Hospitali
hiyo kuwa na uwezo wa kuzalisha idadi
ndogo ya Oksijeni lakini mtambo huo pia umeshaanza kuchakaa kwa sasa hali
ambayo mbeleni itachangia kushindwa kuleta ufanisi.
amesema kutokana njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ni kupatiwa kwa mtambo wa kisasa unaozalisha hewa ya Oksijeni kutokana na kuongezeka kwa mahitaji hayo kila siku.





0 Maoni