KAMPUNI ya kuendeleza matumizi sahihi ya bahari kupitia kamati za uvuvi Zanzibar Marine Costal Community Conservation (MCCC), inamalengo ya kutoa mikopo kwa jamii ya Kisiwa cha Fundo kama motisha kutokana na jamii hiyo kuwa tayari kuendeleza hifadhi ya rasilimali za bahari, ili waweze kujiendeleza katika shughuli nyengine za kiuchumi badala ya kutegemea bahari pekee.

Akizungumza na wananchi wa  Kisiwa cha Fundo katika mkutano wa pamoja wa kutafuta ridhaa juu ya mikopo inayotarajiwa kutolewa, Mkuu wa Program ya Mkuba kutoka -MCCC- Zanzibar  . Fatma Ali Khamis, amesema moja ya malengo ya kampuni hiyo ni kuwawezesha wananchi kuweza kujikwamua na hali ngumu kimaisha.

Kwa upande wa wakufunzi wa Kampuni hiyo, kutoka Wizara ya uchumi wa Bluu, wamewataka wanajamii kuonesha utayari wa kupokea fursa itokanayo na shughuli zao ,ili waweze kunufaika zaidi na miradi inayosimamia rasilimali za bahari.

Nao wanajamii walishukuru kufikiwa na mradi wenye nia ya kuwasaidia kupata maendeleo na kuwaingizia kipato mbadala na kuongeza uzalishaji baharini.