Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akifurahi pamoja na
baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua
Kliniki inayohamishika (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa
serikali ya Mapinduzi ya Waziri wa Afya Ahmed Nassor Mazrui (wa pili kushoto),
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria, Haroun Ali Suleiman (Kulia),
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kushoto) na
Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke
(Kushoto).
Wanafunzi na wakazi wa
Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wakiwa wameketi
pembeni ya Kliniki inayohamishika (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC
kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya
mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo
Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar Raisi Samia ameyasema hayo Jana Agost 28 katika
uzinduzi na makabidhiano ya Kliniki inayohamishika (mobile Clinic) iliyotolewa
na Benki ya NBC kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya
afya hususani ya mama na mtoto visiwani sambamba na kuzindua jengo la madarasa
ya skuli ya maandalizi ya Kizimkazi yaliyojengwa na kukarabatiwa kwa
msaada kutoka Benki hiyo.
Katika hatua nyengine
Rais Samia ametoa wito kwa taasisi hiyo pamoja na taasisi nyingine za kifedha
kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo kwa
wananchi wake.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi alisema msaada huo
wenye jumla ya thamani ya Tsh Milioni 275, ni muendelezo wa
jitihada za benki hiyo za uwajibikaji kwa jamii (CSR)zinazosukumwa na dhamira
kuu ya taasisi hiyo katika kushirikiana na jamii inayoihudumia.
“Benki ya NBC tumekuwa
tukiguswa na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye huduma za afya na elimu hapa
nchini ikiwemo Zanzibar na ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha
tunashirikiana na serikali zote mbili kukabiliana na changamoto zinazohusu
sekta hii muhimu.’’ Alisema huku akibainisha kuwa benki hiyo inaendelea kufanya
jitihada zaidi ili kufanikisha misaada kama hiyo kwenye maeneo mengine
ikiwemo visiwani Pemba.
Alisema huduma
zitakazotolewa na kliniki hiyo kwa akina mama na watoto zitatolewa bure kwa
kuwa zitagharamiwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar .
“Pamoja na msaada huu
benki ya NBC itaendelea kuhudumia vifaa vilivyopo ndani ya kliniki hii hata
pale vitakapokuwa vinapata hitirafu za kiufundi. Tunaamini sasa kupitia huduma
hii wataalamu wa afya wataweza kuwafikia walengwa popote walipo hususani wale
waliopo pembezoni hususani wakina mama na watoto na kupitia msaada wa mwenyezi
Mungu tutaweza kuokoa maisha yao,’’ aliongeza.
Mbali na ujenzi wa
jengo la Madarasa katika wa skuli ya maandalizi Kizimkazi msaada huo
pia umehusisha samani za ndani ya madarasa hayo ikiwemo madawati na meza
sambamba na jiko kwa ajili ya upishi wa chakula cha wanafunzi hao pamoja na
vifaa vya michezo ili kutoa fursa ya watoto kufurahia michezo yao.
Hafla ya makabidhiano
hayo imefanyika Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar
na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, akiwemo Waziri wa Afya Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid
Hadid Rashid, viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)na wananchi wa kijiji
hicho.
Monekano wa jengo la
madarasa ya Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa
kwa msaada wa benki ya NBC.
Mkuu wa Masoko na
Mawasiliano wa NBC, Neema Rose Singo (Kulia) akimkabidhi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan zawadi kwa
niaba ya Umoja wa wanawake wa benki hiyo ikiwa ni ishara ya kumpongeza na
kutambua jitihada za Rais Samia katika kuliongoza taifa.






0 Maoni