Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 11, anaeishi Shehia ya Finya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, amekutwa amejinyonga ndani ya chumba chao kwa kutumia Khanga
Akizungumza na
Sknews Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni
Khatib Yahya amesema tukio hilo
limetokea jana (Agosti 24) majira ya saa 12 jioni katika shehia ya Finya ambapo
hadi sasa Chanzo cha tukio hilo hakijajulikana.
Bi salma amesema
mtoto huyo anaaejulikana kwa jina la Hildat Mohamed Seif anasoma Darasa la Nne
katika Shule ya Msingi Finya ambapo siku ya tukio majira ya saa 10 za join Mtoto huyo alikwenda skuli kwa ajili ya masomo
ya ziada na aliporudi majira ya saa 12 aliingia ndani baada ya muda akakutwa
amejinyonga.
‘‘kiukweli
chanzo cha tukio bado hakijajulikana ila huyo mtoto anaishi na mama yake ambae
kwa kweli nimjamzito kama si wakujifungua leo basi kesho, baba wa mtoto siku ya
tukio hakuwepo Kijijin hapo kwahyo hakukua na mtu aliekua akifuatilia nyendo za
mtoto ’’ amesema bi Mgeni
Amesema kwa
mazingira kwa jinsi ya livyo yanaonesha wazi huenda mtoto huyo amejinyonga ingawa bado polisi wanaendelea na uchunguzi
kubaini chanzo cha tukio lenyewe
‘‘mazingira kwa
jinsi yalivyo inaonesha huenda mtoto amejinyonga maana pale eneo la tukio
linaonesha mtoto alipanda kitandani akajifunga khanga shingoni na kuitupa
khanga kwenye Dari hali iliyopelekea kumkaba shingoni na kusababisha kifo chake’’





0 Maoni