Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Mathew Nkulila (57) ambaye ni Diwani kata
ya Ndembezi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo Jumatatu Agosti 23,2021 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Shinyanga kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.
Nkulila amekuwa Diwani wa kata ya Ndembezi tangu mwaka 2010 na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mwaka 2010-2015.
Nkulila alichaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Novemba 24 Mwaka 2020 na ametumikia nafasi ya Meya kwa kipindi cha miezi 10 hadi umauti ulipomkuta.
David Mathew Nkulila alikuwa na maono ya kuifanya Manispaa ya Shinyanga kuwa Jiji.
Nkulila atakumbukwa kwa misimamo yake thabiti katika kutetea wanyonge, asiyekubali kuyumbishwa na kupiga vita rushwa na ufisadi.
Msiba upo nyumbani kwake mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi jirani na Kanisa la Moravian, taratibu za ratiba za mazishi tutawataarifu.





0 Maoni