Waziri wa Nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa Serikali za mitaa na idara maalumu za SMZ  Massoud Ali  Mohamed akisistiza jambo wakati alipotembelea ujenzi wa jingo hilo Darajani mjini Unguja.
 

Na mwandishi wetu

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais tawala za Mikoa Serikali za mitaa na idara maalumu za SMZ  Massoud Ali  Mohamed amesema utekelezaji wa mradi wa viungo visiwani Zanzibar unachangia  kasi ya maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa wananchi wake hususani kupitia sekta ya kilimo.

 Waziri Massoud aliyasema hayo alipotembelea ujenzi wa jengo maalumu litakalotumika kama sehemu ya kuhifadhia bidhaa za matunda na mboga mboa bila ya kuharibika (Jokofu) pamoja na sehemu ya kufanya biashara za bidhaa hizo katika eneo la Darajani mjini Unguja.

 Alisema wao kama Serikali wamefarijika kwa kiasi kikubwa juu ya uwepo wa mradi huo na kwamba unasaidia kutekeleza ahadi za Serikali kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa sambama na kuongeza idadi ya ajira.

 Pia Waziri huyo alieleza kwa kuwa Soko la Darajani ni moja ya Masoko ya kale Zanzibar hivyo kujengwa kwa jengo hilo jipya kutaacha alama sambamba na kuifanya haiba ya maeneo hayo yenye kuvutia kwa wenyeji na wageni wanaotembeela kila leo visiwani hapa.

 Katika hatua nyengine  aliwataka watendaji wa mradi huo kwa kushirikiana na Baraza la Manispaa kuhakikisha wanawarudisha wafanya biashara wote walioondolewa katika eneo hilo ambalo linatumika kwa ajili ya ujenz huo na sio kufanya vyenginevyo pindi ujenzi wa jesho hilo utakapokamilika.

 Kwaupande wake Meneja Mkuu wa utekelezaji wa mradi huo Amina Ussi Khamis amesema ujenzi wa Soko hilo utagharimu   milioni 342 za kitanzania hadi kukamilika kwake  na unasimamiwa na kampuni ya White Pelican Limited chini ya usimamizi mkandarasi wa ushauri kutoka kutoka kampuni ya ZANPLAN LMITED na hadi kufikia sasa mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 6O.

 Mradi wa utekelezaji mradi wa viungo visiwani hapa unatekelezwa na PDF,TAMWA-ZNZ pamoja na CFP Chini ya ufadhili wa umoja wa ulaya (EU) na utatekelezwa kwa muda wa miaka mine huku ukilenga wanufaika wapatao 57,000 kutoka katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

Meneja Mkuu  utekelezaji mradi wa Viungo Zanzibar Amina Ussi Khamis akitoa maelezo kuhusu lengo la ujenzo wa jingo hilo kwa waandishi wa habari.
Muonekano wa juu ya wajengio hilo kwa ajili ya matayarisho ya ghorofa moja nyengine ukiendelea.