Mbumge wa viti maalum kundi la Wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba Asya Sharif Omar ametoa wito kwa wachezaji  soka kuutumia vyema muda wao kufanya mazoezi kwani soko la soka duniani liko wazi na kila uchao  linahitaji kwachezaji wenye uwezo na vipaji .

Pia alisema kutokana na dunia kuwa kijiji kimoja , mchezaji mwenye uwezo wa  soka, nidhamu na anayejituma ni rahisi kununuliwa toka mahali popote duniani kwa bei kubwa akatajirika.

Asya ambaye ni mwanamichezo ameyaeleza hayowakati akizungumza na Mwandishi wetu kuhusuiana na mtazamo wake katika Masuala ya ajira kwa vijana kupitia soka.

Amesema ni vema wazazi wakawapa nafasi vijana kuishi katika ndoto wanazoziamini kwakua  mpira wa miguu pamoja ni afya na burudani lakini mpira sasa imekua sehemu inayoajiri watu wengi na mafanikio yake ni yamuda mfupi

soka la sasa lina soko kubwa hivyo linatafuta bidhaa ambayo ni wachezaji wenye uwezo  vipaji na uhodari ili wananunuliwe na  timu kubwa za soka duniani.

amesema iwapo wachezaji wa Soka Visiwani Zanzibar watatilia maanani kufanya mazoezi kwa bidii, kujituma na kufuata maelekezo ya walimu anamatumaini makubwa ya kuona Zanzibar ikizalisha wanamichezo wengi watakaotumika katika timu ya Taifa na Vilabu mbali mbali Nchini na Nje ya Nchi.

"Nichukue nafasi kuwataka wachezaji wa soka  wajitambue na kuelewa soka la sasa duniani ni bidhaa muhimu.Ni bidhaa isiokosa soko kwani inahitajika kila uchao duniani. Iwapo wachezaji wa timu zetu watajituma soko la kandanda litawafuata hapa hapa Pemba "Alisema Asya