JAMII imeaswa kupuuza
taarifa za upotoshaji zinazotolewa kwenye mitandao ya kijamii juu ya
chanjo ya UVICO 19 , kwani chanjo hiyo haina madhara kwa binadamu kwa kuwa
imethibitishwa kisayansi na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO.
Ushauri huo umetolewa
na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Salama Mbarouk Khatib wakati akizindua
chanjo wa UVICO 19, na kuwatoa hofu wananchi kwamba Chanjo hiyo haina madhara
kwa binadamu.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya WETE Mgeni Khatib Yahya amewataka wananchi kuendelea kuelimishana umuhimu wa chanjo kwani ni salama.
Awali Afisa Mdhamini Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Yakoub Mohammed Shoka amesema taaluma itaendelea kutolewa ili kuondoa hofu kwa wananchi pamoja na kuwafahamisha faida za chanjo hiyo.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa amewataka viongozi kuwahimiza wananchi kwenda kupata chanjo.
Jumla ya Vituo viwili vya kutolea chanjo vimetengwa kwa Mkoa wa Kaskazini Pemba , amabvyi ni Hospitali ya Wete na Micheweni na vitatoa huduma siku cha kazi.





0 Maoni