Makamu wa kwanza wa
Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman (kulia) akizungumza na Balozi
Mdogo wa Msumbiji(kushoto),anaefanyia kazi zake Zanzibar Balozi Agostinho Abaca
Trinta, aliyefika ofisini kwake Migombani mjini Unguja kwa lengo la
kujitambulisha.Na Mwandishi wetu
Makamu wa kwanza wa
Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema ni wakati wa Serikali kushirikiana na nchi ya Msumbiji katika kuikuza sekta ya mafuta na
gesi kwa ajili ya kuuinuwa uchumi wa Zanzibar kupitia sekta hiyo.
Mhe. Othman ameyasema hayo (Agosti 4) wakati akizungumza na Balozi Mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar, Balozi Agostinho Abaca Trinta, aliyefika ofisini kwake Migombani mjini Unguja kwa lengo la kujitambulisha.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Othman amesema Msumbiji ni Nchi iliyopiga hatua katika sekta ya Mafuta na Gesi na hivyo pande hizi mbili zinaweza kubadilishana ujuzi na kuona namna ya kuikuza zaidi sekta hiyo.
Amesema Mafuta na Gesi ni miongoni mwa sekta ambayo kwa sasa Serikali ya Zanzibar inaipa kipaumbele kwa lengo la kuona inaongeza maeneo yatakayosaidia katika kukuza uchumi wa nchi.
Naye Balozi Agostinho Abaca Trinta, akamuhakikishia Mhe. Othman kuwa nchi hiyo itaendelea kuwa pamoja na kukuza uhusiano wake na Zanzibar, ili kuona zinafikia maendeleo, pamoja na kueleza salamu za Rais wa nchi yake Mhe. Filipe Nyusi, zakusisitiza umoja na mshikamano kati yao na Zanzibar.




0 Maoni