Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mara baada ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika
leo tarehe 18 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo
Jijini Lilongwe nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce
Banda mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Lilongwe nchini Malawi leo
tarehe 18 Agosti, 2021.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Bi. Joyce Banda Lilongwe nchini Malawi. Rais Mstaafu Joyce Banda alifika Lilongwe kuzungumza na kumpongeza Rais Mhe. Samia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili Zanzibar wakati
akitokea nchini Malawi ambapo alishiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo
tarehe 18 Agosti nchini Malawi.

Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa
Rais Mhe. Dkt. Phillip Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18
Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi
mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
0 Maoni