Mwonekano wa gari lililokuwa limewabeba maofisa wadhamini na kupata nayo ajali katika eneo la Pandani Pemba Na Mwandishi wetu
Maofisa wadhamini Watatu wamenusurika kifo baada ya kutokea
ajali ya gari asubuhi ya leo Agosti 30
katika eneo la Pandani skuli, Shehia ya Pandani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya gari walilokua
wakisafiria kupoteza mwelekeo kutokana
na kupasuka kwa gurudumu la mbele.
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahya ambae alikua katika eneo la tukio amesema ndani
ya gari hiyo iliyopata ajali ilikuwa inajumla ya watu wanne, maofisa wadhamini
watatu na dereva aliekuwa akiendesha gari hilo ila wote wamefanikiwa kutoka
salama
Mhe Mgeni amesema
baada ya ajali hiyo, majeruhi wote
waliwahishwa katika Hospitali ya Micheweni kwaajili ya uchunguzi zaidi na baada
ya Vipimo wote walionekana wazima na majira
ya saa saba za mchana waliruhusiwa kurudi nyumbani.
waliojeruhiwa katika
ajali hiyo ni Ahmed Abubakar Mohamedi ambae
ni Afisa mdhamini Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Raisi, wengine ni Aly Salum Mata
Afisa mdhamini Ofisi ya Raisi, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara
Maalum za Smz na Abdulwahab Bakari ambae ni Afisa Mdhamini Wizara ya Fedha na
Mipango na Dereva wa gari hili ambae jina lake hatukulipata.
Wakizungumza na sknews
wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema maeneo ya Pandani skuli sio salama kwakua pamekua pakitokea ajali za
mara kwa mara na wao wamekua wakizishuhudia bila kujua sababu ya eneo hilo
kutokea ajali nyingi.
0 Maoni