Meneja wa Hifadhi ya Kisiwa cha Mnemba na Ghuba ya Chwaka Mohd Chum Juma kutoka Idara ya hifadhi za maeneo ya bahari amewataka Manahodha wa boti za kuchukulia watalii kuwa na utaratibu mzuri wanapofanya shughuli zao za kitalii bila ya kuharibu rasilimali za bahari.

 Meneja Juma ameyasema hayo August 10  alipokuwa na kikao cha pamoja na Manahodha wa Vijiji vya Mbuyu Tende,Tundangaa na Kigomani juu ya kufuata sheria zilizowekwa na Serikali huko Matemwe Kaskazini Unguja.

 Meneja Juma ameongezea kusema lengo kuu la kuhifadhi maeneo ya bahari ni kutejesha haiba ya visiwa vya Zanzibar na rasilimali zake pamoja na viumbe vilivyoadimika kwa sasa.

 Katika hatua nyengine Mohamed amesema Manahodha wote wanaotembeza wageni visiwani  wawe na utaratibu wa kuwa na vifaa vya usalama kama Maboya, Box la huduma ya kwanza na Makoti(life jacket) ili kuchukua tahadhari za kiusalama kwa wageni pale linapotokea tatizo.

 Nao Manahodha wa wanaotembeza wageni katika kisiwa cha Mnemba wamesema kuwa wameyapokea maagizo kutoka Serikalini huku wakiahidi kuyafanyia kazi

 Hata hivyo wameomba serikali kuwawekea Maboya kwa lengo la kufungia nanga ili kulinda matumbawe ya samaki na rasilimali nyenginezo.