Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Godfrey Nyaisa  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya maafisa Biashara kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, jijini Dodoma  Agosti 16, 2021.

Na mwandishi wetu

Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  iko mbioni kunzisha mpango wa malipo ya maombi  ya biashara kwa njia ya mtandao kwa lengo la kupunguza usumbufu kwa wapokea huduma.

Mpango huo umetangazwa rasmi hii leo Augost 17 na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Godfrey Nyaisa  wakati akifungua  mafunzo  ya siku tano ya maafisa Biashara kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, jijini Dodoma.

Amesema kuwa lengo la mpango huo ni kurahisisha utendaji Kazi  na kuwadhibiti maafisa wabadhilifu wa fedha za umma ambao baadhi walikuwa wanajitengenezea vitabu feki vya leseni.

Nyaisa amesema kuwa hivi sasa maombi yote ya leseni yatakuwa kwenye mfumo mmoja ambapo mfanyabiashara atakuwa anaomba leseni kupitia kwenye mtandao na kulipia kwa kutumia namba maalumu ya malipo serikalini (Control Number) na kwamba mpango huo utapunguza kwa asilimia kubwa ubadhirifu hivyo kuongeza wigo wa mapato.

"Serikali ina shida na mfanyabiashara na mfanyabiashara ana shida hivyo msikurupuke kuwafungia biashara, kaeni muelewane, mtumie busara lakini pia mkae mkijuwa kuwa licha ya Serikali kutaka mapato lakini kazi yake kubwa ni kutoa huduma," amesema Nyaisa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Godfrey Nyaisa  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya maafisa Biashara kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, jijini Dodoma  Agosti 16, 2021.
                     maafisa biashara wakifuatilia kwa ukaribu masomo