Matajiri wa Jangwan Klabu ya Yanga Sc inadaiwa kuwa imevunja
ndoa yake na mchezaji wake Juma Makapu ambaye ameitumikia klabu hiyo
kwa muda mrefu.
Makapu amekuwa na kikosi cha Yanga Sc kwa Zaidi ya
Misimu Mitano lakini ameshindwa kushawishi walimu kutumika katika kikosi cha
kwanza.
Makapu mwenye uwezo
wa kucheza kwa ufasaha nafasi ya kiungo mkabaji, beki ya kati na kulia,anahusishwa
na kusajiliwa na Timu ya Mtibwa Sukari yenye Makao yake Makuu Turiani Mkoani
Morogoro
Juma Makapu alijiunga na Yanga kwa Mra ya Kwanza mwaka
2014 akitokea katika Klabu ya Shangani Visiwani Zanzibar wakati huo yanga
ikinolewa na Kocha Mwenye asili ya Kibrazil Marcio Maximo.





0 Maoni