MAKAMU wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka watendaji wa Sense ya watu
na Makazi kuwanawafikia viongozi wa kisiasa na vyama vyao ili kufikishia vema
wananchi ujumbe wa elimu ya sensa ya watu na makaazi.
Mhe Masood ameyasema
hayo leo ofisini kwake Migombani alipokutana na Kufanya mazungumzo na Kamisaa
wa Sensa ya Watu na Makaazi Zanzibar,
Balozi Mohammed Hamza pamoja na watendaji wa Sensa ofisi ya Zanzibar.
Amesema kufanya hivyo
kutasaidia wananchi kupata elimu sahihi juu ya Sensa ya watu na makaazi
inayotarajiwa kufanyika Ogasti mwaka ujao ili ofisi hiyo iweza kukabiliana na
baadhi ya changamoto za uwelewa kwa wananchi kuhusu suala la sensa.
Amesema ni vyema
wananchi wakaelimishwa ili wafahamu kwamba kushiriki katika sensa ni uwekezaji
muhimu katika upangani na uwekaji wa mipango sahihi ya maendeleo ya Zanzibar.
Naye Kamisaa wa Sensa
Zanzibar Balozi Mohammed Hamaza amemueleza makamu kwamba mandalizi ya sensa hiyo yanaendelea
ikiwa ni pamoja ukataji wa maeneo ya kuhesabu watu .
Balozi Hamnza
alifahamisha sensa ijayo tafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili
kuwezesha kukusanywa kwa usahihi takwimu mbali mbali zinazohusu idadi ya
watu, makaazi, shughuli za kijamii na
mambo mengine mbali mbali.





0 Maoni