Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed
Suleiman Abdulla akimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari kuchukua
hatua za haraka ndani ya Kipindi cha wiki moja kufanya marekebisho ya
Miundombinu katika maeneo mbali mbali ya Bandari ya Malindi.
Na mwandishi wetu
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed
Suleiman Abdulla ametoa muda wa siku Kumi (10) kuangamiza au kurejesha
zilipotoka bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi.
Mhe. Hemed alitoa agizo hilo wakati alipofanya
ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Malindi Jijini Zanzibar.
Katika ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar alitembelea ghala lililohifadhiwa mafuta lainishi (Oil) ambayo
yaliingizwa nchini mwaka 2019 kutokea Dubai na kukosa kiwango Kwa matumizi ya
Vyombo vya Moto.
Alisema ni vyema kwa wizara kuhakikisha
Zanzibar haipokei bidhaa zilizopitwa na wakati kwa usalama wa wananchi wake,
Pamoja na kuitaka wizara ya Biashara na maendeleo ya Viwanda kuchukua hatua
kali kwa wafanyabiashara wanoingiza Bidha zilizopitwa na wakati ili iwe
fundisho kwa wafanyabiashara wengine.
“ Zanzibar sio sehemu ya kuja kutupa bidhaa
zisizo salama, Naitaka Wizara ya biashara na maendeleo ya viwanda kuhakikisha
wanachukua hatua kali kwa wahusika wanaoleta bidhaa hizo kwa kufuata
sheria na taratibu” Alisema Makamu wa Pilin wa Rais
Katika ziara hiyo Mhe. Hemed alikagua mchele
aina ya Asha Kuku ulioletwa na kampuni ya A.R.Y ulioingia Zanzibar
July 11, mwaka huu na na mchele ulioletwa na I.A SIWJE TRADERS ulioingia
Zanzibar June 30 mwaka huu, ukiwa ni jumla ya kontena 10 sawa na tani Mia
mbili na Sitini (260).
Mhe. Hemed Alitaka mamlaka ya kuzuwia
Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) kumaliza kesi ya mchele wa I.A
SIWJI TRADER ambapo kampuni hiyo imeashiria kutenda
vitendo vya uhujumu uchumi kwa kutoa rushwa ili kuhalalisha bidhaa yake
ilikwisha pitwa na muda.
Akitoa taarifa kuhusu bidhaa ya mafuta
lainishi Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Viwango Zanzibar (ZBS) Ndugu Muhamed Mwalim
Simai alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa bidhaa hiyo
ilikaguliwa na TBS na kukataliwa na hatimae muhusika huyo kuhamishia Zanzibar
Bidhaa hiyo ambapo ZBS imeizuiwia kuingia sokoni.
Kwa Upande wake Mkuu wa Usajili na Tathmini ya
Chakula kutoka ZFDA Ndugu Khadija Ali Sheha alimueleza Makamu wa Pili wa Rais
kuwa mchele uliongizwa Zanzibar kutoka Kampuni hizo umeshafanyiwa vipimo
na kuonekana kupitwa na wakati sambamba na kugundulika kuwa haufai kwa matumizi
ya binadamu ambapo Mamlaka yao imetoa maelekezo kwa wahusiku kuweza
kuchukua hatua zaidi.
Katika ziara yake Makamu wa Pili wa Rais
alikagua eneo la kumpunzikia abiria, Ofisi ya Uhamiaji, Ofisi ya wakaguzi wa
Afya na kutoridhishwa na Mazingira ya maeneo hayo.




0 Maoni