Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Ameeleza kusikitishwa kwake kwa kuona baadhi ya Vituo vya Afya Nchini vikiendelea kukosa vitendanishi (Reagents) na baadhi ya huduma wakati Ghala la Bohari kuu limesheheni mzigo mwingi wa dawa na vifaa vya kutosha vinavyohitajika katika vituo vya Afya.

Mhe. Hemed ameeleza hilo leo (augusti 11) katika ziara ya kushtukiza aliyoifanya Bohari kuu ya dawa iliyopo Maruhubi Jijini Zanzibar

Amesema si vyema wananchi kulipia huduma za Afya nje ya vituo vya Serikali kutokana na  kugharimu kiasi cha fedha kupata huduma hiyo ilhali huduma hiyo kuna uwezekano wa kupatikana kwa Hospital za Serikali.

Mhe Hemed ameuagiza uongozi wa Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar kusambaza vitendanishi (Reagents) katika vituo vya afya vyenye uhitaji ili kuwaondelea usumbufu wananchi wanaohitaji huduma iyo.

Katika hatua nyengine mhe Hemed amemuagiza Mkugenzi Mkuu Wizara ya Afya kutowavumilia na kuwachukulia hatua watendaji wanaochelewa kuagiza dawa Bohari kuu kwani kufanya hivyo kunawachelewesha wananchi kupata huduma stahiki.

Wakieleza changamoto wanazokumbana nazo wafanyakazi wa bohari hiyo wamemueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa ucheleweshaji wa maombi ya dawa kutoka vituoni hupelekea kuchelewa kwa usambazaji wa dawa zinazohitajika, jambo ambalo linapelekea wananchi kupoteza imani na serikali yao.

ANGALIA TUKIO ZIMA KATIKA ZIARA YA KUSTUKIZA YA MAKAMO WA PILI WA RAIS