Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo ambae pia ni Makamo wa kwanza wa Raisi
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Othman Msoud Othman amesema
ataiendeleza kwa Juhudi na hekma kubwa kazi iliyofanywa na Mtangulizi wake
marehemu Maalim Seif Sharif Hamad katika kuhakikisha Zanzibar inapata
maendeleo.
Mhe.
Othman ameyasema hayo Kisiwani Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati akizungumza
na wananchama wa Chama hicho katika ziara rasmi ya kujitambulisha katika jimbo hilo .
Amesema
ni vema wananchi wakaendelea kutekeleza jambo muhimu la kujenga umoja kama
lilivyo asisiwa na mtangulizi wake ili
kuungana na viongozi wa kitaifa katika juhudi kubwa wanazozifanya za
kuunganisha watu na kupigania haki na
maendeleo.
‘‘
wananchi wanapaswa Msivunjike moyo
kwakua viongozi wenu tunajitahidi kupigania uwajibikaji na uwadilifu katika
Serikali kwa kuwa ndio njia muhimu zaidi
ya kuleta maendeleo ya Zanzibar’’
Katika
hatua nyengine Mhe Othman amesema Chama
hicho kushiriki
katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa kumetokana na hekima na maauzi ya chama
hicho na kwamba kazi ya kusimamia suala hilo alilokabidhiwa ni jambo kubwa na
ataifanya kwa juhudi na hekima kubwa ili wananchi wa Zanzibar wamapete
maendeleo kama ilivyokusudiwa.
Mapema
Mhe. Othman alikutana na wazee wa Chama cha ACT Jimbo la Tumbatu kwa nia ya
kujitambulisha kwa wazee hao kutokana na kukabidhiwa jukumu kubwa la uongozi wa
Zanzibar.
Katika
ziara hiyo Mhe. Othman aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mhe.
Juma Duni Haji,Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar
Salim Biman, Naibu Katibu wa Idara ya Organizetion, Omar Ali Shehe pamoja na
viongozi wengine mbali mbali.
0 Maoni