Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar akikagua maeneo mbali mbali katika Hospital ya
wagonjwa wa akili ya Kidongochekundu kufuatia ziara ya kushtukiza alioifanya
leo kwa ajili ya kujionea huduma zinazotolewa kwa wananchi.Na mwandishi wetu
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka uongozi wa
Wizara ya Afya kutatua changamoto ya kukosekana kwa Vifa tiba katika Hospital
na vituo vya Afya Nchini Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa
wananchi.
Mhe.
Hemed ameeleza hayo katika ziara yake ya kushtukiza Hospitali ya
Mwembeladu na Hospital ya Wagonjwa wa akili Kidongo Chekundo kwa lengo la
kujionea huduma zinavyotolewa kwa wananchi wanaofika katika Hospitali hizo.
Amesema
viongozi wenye dhamana ya kusimamia vituo vya Afya wana jukumu la kuhakikisha
vifaa tiba vinavyohitajika vinapatikana kwa wakati sambamba na kufanya
ukarabati wa maeneo mbali mbali ili kuweka mazingira bora kwa wafanya kazi
wanaotoa huduma kwa wananchi.
Wakati
ametembelea Hospital ya Mwembeladu Makamu wa Pili wa Rais amesema maeneo ya
kufanyia kazi kwa madktari katika hospital hiyo sio ya kuridhisha, hivyo
amemuagiza Mkurgenzi Mtendaji wa Hospital ya Mnazi Moja Dk. Msafiri Marijani
kuchukua hatua za haraka kwa kufanya ukarabati wa kawaida katika baadhi ya
maeneo.
Akikagua
sehemu ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba Mhe. Hemed alimuelekeza Dk. Marijani
kuhakikisha vifaa tiba ikiwemo mikoba ya kujifungulia pamoja na dawa muhimu
zinazopatikana katika bohari kuu ya Serikali zinapatikana kwa wakati katika Hospital
hizo.
Mmoja ya wananchi waliofika katika Hospital ya Mwembeladu akimueleza Makamu wa Pili wa Rais changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kukosekana kwa kipimo cha damu katika Hospital hiyo.




0 Maoni