MAKAMO wa Kwanza wa
Rais Zanzibar Mhe Othman Massoud Othman amelitaka shirika la Biashara la Taifa
Zanzibar-ZSTC- Kujiendesha kibiashara na kuondoa dhana ya kwamba shirika hilo
linatoa huduma kwa wakulima wa zao la karafuu.
Akizungumza katika mkutano wake na wadau wa karafuu Kisiwani Pemba , ambapo Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe Othamn Massoud Othman anatumia fursa hiyo kulitaka shirika Biashara la Taifa Zanzibar-ZSTC- kufanya mageuzi na kuja na dhana ya biashara na sio dhana ya kutoa huduma.
Aidha Makamo wa Kwanza ameshauri kuanzishwa chombo huru kinachoamua daraja la karafuu ili kuondoa malalamiko ya wakulima.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Salama Mbarouk Khatib amewataka wadau hao wa karafuu kushirikiana na serikali kukomesha vitendo vya wizi wa karafuu
Hata hivyo wadau wa karafuu Kisiwani hapa wameitaka serikali kuandaa utaratibu ambao utawawezesha kutambua viwango na madaraja la karafuu .





0 Maoni