MKUU wa Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo KMKM Zanzibar Komodoo Azana Hassan Msingiri ametangaza kupeleka vifaa Pamoja na Askari katika eneo la Moa Mkoani Tanga , eneo ambalo linadaiwa kutumiwa kupitisha biashara haramu ya magendo ya karafuu.

 Komodoo Msingiri ameyasema hayo wakati akizungumza na masheha wa Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo amesema eneo la Moa litawekwa vyombo Pamoja na Askari wa kutosha ili kudhibiti biashara hiyo haramu.

 Mkuu Wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amesema marufuku ya kusafirisha karafuu majira ya usiku itaendelea ili kuzuia utoroshaji kwa baadhi ya wananchi wasio waaminifu.

Kwa upande wa wakuu wa Wilaya ya Wete na Micheweni wamewataka masheha kujiepusha na vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara ya magendo.