Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo (KMKM) COMMODORE Azana Hassan Msingiri akimkaribisha Mtendaji mkuu  Ofisi ya Rais  Ikulu (Mlikulu) Mahmoud Othman mara alipofika Ofisini hapo  kwaajili ya kuopokea samaki waliovuliwa na kikosi hicho kwaniaba ya Rais wa Zanzibar Huko Ofisi za (KMKM)  Kibweni Zanzibar.

Mkuu wa Doria Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo (KMKM)  Kamanda Hussein Ali Makame akimkabidhi samaki aina ya Jodari Mtendaji mkuu  Ofisi ya Rais  Ikulu (Mlikulu) Mahmoud Othman kwa niaba ya Mkuu wa Kikosi hicho  COMMODORE Azan H. Msingiri ikiwa ni zawadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Na Mwandishi wetu

Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) kimeeleza kuwa kinathamini na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuinua uchumi kupitia Bahari kuu.

Mkuu wa Kikosi cha KMKM Zanzibar, Commodore Azana Msingiri amesema kikosi hicho kimejipanga katika kuimarisha upatikanaji wa samaki wakubwa kwa kutumia vifaa na uvuvi wa kisasa ili kufikia azma ya serikali ya Uchumi wa Buluu.

Amesema katika kipindi cha majaribio Kikosi hicho kimevua samaki wakubwa katika bahari ya Zanzibar ikiwemo aina ya jodari na papa.

Commodore Msingiri ameeleza hayo katika hafla ya kukabidhi samaki waliovuliwa na kikosi cha (KMKM) Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha ameeleza kuwa kikosi chake kimepanga kupeleka watendaji wa kikosi hicho pamoja na vifaa Kisiwani Pemba kwa ajili ya doria ya kudhibiti magendo ya karafuu katika kipindi hichi cha uchumaji wa zao hilo unaoendelea.

Nae Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais Ikulu (Mlikulu) Mahmoud Othman ameikipongeza kikosi cha KMKM na kukitaka kuimarisha doria ili kuepukana na magendo.

Kwa upande wake Kamanda Hussein Ali Makame Mkuu wa doria KMKM amesema kikosi kinafanyakazi kwa vitendo katika kuimarisha uchumi wa buluu pamoja kuzuia magendo nchini.