Akizungumza bungeni Jijini Dodoma hii leo Mwenyekiti wa Kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge Emmanuel Mwakasaka, amesema kuwa mbunge Josephat Gwajima amekutwa na hatia baada ya Kamati ya maadili kumuhoji juu ya shutuma zinazomkabili na kisha kukiri kuwa maneno aliyoyatoa ni ya kwake mwenyewe na kwamba alikuwa akiwahubiria waumini wake ulimwenguni kote kuhusiana na janga la Covid-19 na chanjo ambazo zinatolewa
Itakumbukwa kuwa Gwajima amekuwa akitumia Kanisa
lake la Ufufuo na Uzima kwa kuikosoa serikali ya Tanzania kuhusu chanjo ya
Corona zinazoendelea kupigwa nchini kwa kile alichodai kuwa chanjo hiyo ni nia
mbaya ya Mataifa ya magharib kwa Tanzania, huku akionekana kwenda kinyume na
Rais wa nchi na viongozi wengi wa serikali katika uhamasishaji wa uchomaji
chanjo hiyo.





0 Maoni