Mahakama ya Kisutu imeahirisha Kesi ya Ugaidi inayomkabili
Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema Freman Mbowe na wenzake
watatu hadi Agosti 13, 2021.
Kesi hyo imeghairishwa baada ya upande wa Serikali kudai taratibu za kuifungua kesi hiyo katika Mahakama yenye mamlaka ya kuisikiliza kutokamlika.
Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo leo Ijumaa,
Agosti 6, 2021 asubuhi wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa
na magari mawili ya wazi yenye askari magereza.
Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya
Mahakama. Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire,
Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.





0 Maoni