Imamu mkuu wa Ghana, Shehe Osman Sharubutu
amechangia zaidi ya $8,000 (£5,800) ili kusaidia ujenzi wa kanisa kuu la
kitaifa lenye utata.
Taifa hilo lina historia ya kuwa na mahusiano mazuri
ya amani ingawa hatua ya kiongozi wa dini kuchangia fedha nyingi kwa imani
nyingine si jambo la kawaida.
Imamu mwenye umri wa miaka 102-amesema ameamua
kufanya jambo hilo ili kuimarisha amani ambayo ipo kati ya wakristo na
waislamu.
Miaka miwili iliyopita kiongozi huyo alihudhuria
ibada ya Pasaka katika kanisa katoliki na kusababisha gumzo kwenye mitandao ya
kijamii.
Kwa sasa serikali imezindua ujenzi wa kanisa na
kuwasisitiza Waghana wachangie katika ujenzi huo, kanisa hilo linajengwa katika
mji mkuu wa Accra, na gharama za ujenzi zinatarajiwa kuwa zaidi ya dola milioni
100.
Ujenzi wa kanisa hilo la taifa unatarajiwa kumalizika mwaka 2024, ikijumuisha na makumbusho ya biblia na ukumbi unaoenea viti 5,000.





0 Maoni