Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Suzan Kunambi amewataka  Madiwani wa Manispaa hiyo, kusimamia  vyema vyanzo vya mapato ili kufikia malengo ya Serikali  katika kukuza uchumi na kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Akifungua kikao cha Madiwani wa Manispaa ya Magharib A  cha utekelezaji  kwa kipindi  cha robo ya nne April/  June 2020/2021 kwenye  ukumbi wa Manispaa amesema ukusanyaji unaofanywa kwa njia ya kieletroni utaweza kuleta mabadiliko  na kuuzuia mianya ya upotevu  wa fedha kupitia vianzio vyake.

 Nae kaimu Mkurgenzi wa Manispaa ya Magharib A, Amour Ali  Abdullah  akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa  robo ya nne ya kikao cha mabaraza ya   Madiwani  amesema kwa kindipi  kifupi   wameweza kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo mpya wa ukusanyaji na kufikia  asilimia 7 sawa na Shilingi Milioni Mia  mbili  themanini na Tatu, Laki Sita Tisini  Nne  Elf  na Mia  nne   themanini na sita (Tz sh.283,694,486) ambavyo vinatokana na vianzio  vyake vya ndani 

 Akizungumza  kwa niaba ya Madiwan wenzake Diwani viti maalum Khaitham  Muhdini Khamis  amesema  wamejiunga kupitia kamati yao ya sheria  na utawala  kwa kusimamia vyema majukumu yao kwa  maslahi ya jamii.