Klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara zimekubaliana kwa kauli moja, Ligi Kusimama kila ambapo Timu za Tanzania zinazoshiriki Michuano ya Kimataifa wanapokuwa na michezo ya Kimataifa ili kuondoa viporo kwa baadhi ya Timu hasa zitakazokua zinashiriki CAF Champions League na CAF Confederation

Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Pamoja kati ya Viongozi wa Bodi ya Ligi na Wenyeviti wa Timu zinazoshiriki Ligi kuu kwa msimu ujao waliokutana hii leo Agust 6,2021

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo amesema katika msimu Mpya wa ligi kwa mwaka huu wamedhamiria kukomesha viporo jambo ambalo limekubaliwa na Wenyeviti wa Vilabu vyote vya Ligi Kuu.

Utaratibu huu Mpya utakapoanza kutumika utapunguza malalamiko kutoka kwa wadau wa soko ambao katika Misimu kadhaa sasa kumekua na malalamiko kutokana na baadhi ya Vilabu vinavyoshiriki Michuano ya Kimataifa kifikia kuwa na viporo hata sita jambo ambalo limeelezwakusababisha kukosa uwiano mzuri wa mashindano