Mkuu wa Chuo Kikuu cha St. Augutine cha Tanzania (SAUT) tawi la Dar es salam Ananias Aloys Rutambuka akizungumza na wanahabari  katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni,

 Na mwandishi wetu

Chuo Kikuu cha St. Augutine cha Tanzania (SAUT) kinatarajia kuanzisha tawi lake Zanzibar kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini.

 Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa chuo hicho tawi la Dar es salam Ananias Aloys Rutambuka  katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni, amesema kuanzishwa tawi hilo Zanzibar itasaidia kuondoa usumbufu wa wanafunzi kufuata elimu ya juu katika maeneo ya mbali

Amesema tayari wameshaanza kufanya taratibu za kusajili tawi hilo kuwepo Zanzibar kwa kufuata kanuni zilizowekwa ili kuanczishwa chuo hicho.

Amesema kuwa vyuo vya elimu ya juu ni muhimu kwani vinasaidia kuleta maendeleo na uwataka vijana wa Zanzibar kujiunga na vyuo vya Elimuya juu ili kujifunza kitaaluma.

“Katika kupambana na Sayansi na Technolojia iliyopo  lazima watanzania wajiendeleze zaidi kielimu  ili kufikia malengo waliyojiwekea hivyo ni wajibu wa vijana kujiunga katika vyuo mbalimbali vilivyopo nchini”, amefahamisha Mkuu huyo.

Mkuu huyo wa Chuo amewasisitiza vijana wanaotaka kujiendeleza kielimu  kuomba  mikopo katika Bodi ya Mikopo kwa lengo la kuwasidia  kimasomo zaidi  pamoja  na kulipa deni baada ya kumaliza masomo yao ili na wengine wanufaike.

Nae mhitimu wa Chuo cha SAUT Suleiman Abdallah ambae pia ni mwandishi wa habari amewashauri wanahabari kujiunga na chuo hicho ili kuendeleza fani zao na kuweza kufanyakazi kiufanisi zaidi.

CAPTION: Mkuu wa chuo  kikuu cha St .Augutine cha Tanzania (SAUT) tawi la Dar es salam Ananias Aloys Rutambuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanafunzi kujiunga na elimu ya juu nchini katika Ukumbi wa Wizara  ya Utalii na Mambo ya kale Kikwajuni Mjini Zanzibar .